Mkutano Mkuu wa IRMT 2018, Stella Maris – Bagamoyo

TAASISI ya vihatarishi nchini (IRMT) imetakiwa kutokufumbia macho udukuzi wa mitandao (data)  wakuwa ni hatari katika kukua kwa uchumi. Imeelezwa kuwa udukuzi wa data ni hatari katika kukua kwa uchumi wa nchi kwakuwa mikakati mingi ya kimaendeleo inafanywa katika mifumo ikiwemo udhibiti wa rushwa, ubadhilifu na udanganyifu.

Akizungumza jana Mjini Bagamoyo Mkuguzi Mkuu wa Ndani wa serikali, Mohamed Mtonga, katika Mkutano Mkuu wa IRMT alisema kukua kwa teknolojia nchini kuna changamoto nyingi hivyo ni lazima kujipanga katika kudhibiti vihatarishi vya kiuchumi ikiwemp udukuzi wa mitandao.

“Katika matumizi ya teknolojia kuna matatizo mengi hivyo ni lazima kudhibiti vihatarishi vilivyopo ili kuweza kufikia malengo ya uchumi wa kati,”alisema.

Alisema uchumi huo wa kati unasukumwa na uanzishaji wa viwanda hivyo udhibiti wa vihatarishi ni muhimu.

Mtonga aliongeza kuwa katika mkutano huo wamejadili kwa kina hatua uchumi kukua kwa kasi na namna watakavyokabiliana na vihatarishi katika sekta ya mafuta na gesi.

Aliongeza kuwa kufanya vizuri kwa taasisi hiyo kunaweza kupunguza uhaba wa wataalamu wa vihatarishi uliopo na kusaidia kukua kwa pato la ndani la taifa.

“Kama tutaungana na serikali iliyopo kuhakikisha tunazalisha wataalamu wazalendo ambao ni watendaji wenye maadili, watasaidia katika kuminya

matumizi yasiyo ya lazima, kudhibiti ubadhilifu na kukuza pato la ndani la taifa,”alisema.

kwa upande wake Rais wa taasisi hiyo Pius Maneno alisema umuhimu wa kukutanisha watalamu kutoka ndani na nje ya nchi wa sekta binafsi na serikali katika sekta ya vihatarishi ni muhimu katika kulinda uchumi.

Alisema ili bajeti na maendeleo yaweze kufanikiwa ni lazima kudhibiti vikwazo vya kiuchumi.

“Huu ni mkutano wetu wa kwanza na tutahakikisha tunakutana ndani na nje ya nchi ili kujengeana uwezo wa kufanikiwa kudhibiti vihatarishi vyote vya maendeleo,”alisema.

Alisema changamoto zinazozikabili nchi za Afrika katika maendeleo ni nyingi hivyo ipo haja kuwa na mikakati endelevu.

[wzslider autoplay=”true”]

Add a Comment

Your email address will not be published.